Homa ya mechi ya watani wa jadi imepanda. Simba inaondoka Dar es Salaam leo Jumatatu kwenda Zanzibar kuweka kambi lakini wenzao Yanga wanatokea Shinyanga kuelekea Morogoro.


Simba na Yanga ambazo zinacheza Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, zimeanza harakati za kuwindana kila mmoja akijiweka sawa kwa pambano hilo ambalo ni turufu muhimu kwa ubingwa.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema; "Tuna mechi ngumu  dhidi ya Yanga, tutaondoka wote kuelekea Zanzibar katika kambi ya pambano la watani," alisema.

Mara ya mwisho Watani hao walikutana katika mechi ya Ngao ya Hisani ambapo Simba ilitokea Unguja na Yanga kisiwa cha Pemba na Simba kuibuka na ushindi wa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana.

Habari za uhakika kutoka Shinyanga zinasema kwamba Yanga safari hii haitakwenda Zanzibar bali itakwenda kutulia Morogoro mpaka siku moja kabla ya mechi ya watani ambayo ni Ijumaa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: