Mcheza Kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet, anatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi ya Kikapu nchini Japan akiwa na timu yake ya Yokohama B.


Hasheem amesajiliwa na klabu ya Yokohama B, Septemba 28, mwaka huu  inayoshiriki Ligi Kuu ya mchezo wa kikapu nchini Japan ‘B1 League’ atatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Levanga Hokkaido katika dimba la kimataifa la Yokohama ‘Yokohama International Arena Pool’.

Mchezo huo wa kwanza kwa Thabeet ambaye amewahi kucheza kwenye ligi ya Kikapu nchini Marekani (NBA) utapigwa Oktoba 7 siku ya Jumamosi ya wiki hii.

Thabeet aliichezea klabu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi ya Marekani ‘NBA’ jumla ya michezo 224 ikiwa ni sawa na wastani wa pointi 2.1 na mitupo 2.6 “rebounds”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: