
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, ametoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 3,284 wa jimbo lake huku akisema amefanya hivyo kwa kuwa wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu na sasa ni vyema vijana wakawahudumia.
Utoaji wa vitambulisho hivyo ni utekelezaji wa Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee, ambapo baada ya kupata vitambulisho hivyo, itakuwa rahisi kwao kwenda hospitali na kupatiwa matibabu bila malipo.
Katika uzinduzi wa zoezi hilo, Bashe ametoa vitambulisho 540 na vingine vitaendelea kutolewa katika ofisi ya Mbunge iliyopo Nzega Mjini.
Akizungumza na wazee waliojitokeza kupokea vitambulisho hivyo, Bashe alisema: “Wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu, ni jukumu letu sasa kama vijana na Taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia matibabu bora na kuwaondolea gharama za matibabu ili kuleta unafuu wa maisha.
“Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za vitambulisho ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini anapata kitambulisho cha matibabu ya bure.”
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi hilo, alimpongeza Bashe kwa kusimamia shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote.
Post A Comment: