KOCHA wa muda wa timu ya soka ya Taifa ya Uganda, Moses Basena, ameita viungo wawili wapya kuimarisha kikosi chake kitakachoikabili Ghana katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia itakayofanyika mwezi ujao huku akimwacha beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid.


Viungo wapya walioitwa ni Tony Mawejje na Geoffrey Kizito, ambao walikosa mechi zilizopita dhidi ya Misri, moja walishinda wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mandela (zamani Namboole) uliopo jijini Kampala.

"Ninafuraha kuona Mawejje sasa amepata nafasi ya kucheza, atakuwa mchezaji muhimu kwenye kiungo katika mechi dhidi ya Ghana," Basena aliiambia KweséESPN.

Onyango aliiambia KweséESPN kuwa uwepo wa Mawejje kwenye kikosi hicho ni muhimu.

Aliongeza: "Tulipata tabu sana kumkosa kwenye timu tangu alipoitumikia nchi mapema mwaka huu.

"Ingawa tutamkosa Aucho na Murushid Juuko kwa sababu ya kutumikia kadi za njano, bado tuna kikosi imara ambacho kinauwezo wa kutupa matokeo mazuri."

Mchezaji mwingine wa Uganda anayecheza katika Ligi Kuu ya Tanzania aliyeitwa kwenye kikosi hicho cha Uganda ni mshambuliaji, Emmanuel Okwi ambaye anaongoza kwenye ufungaji.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: