ads

Timu ya soka ya Simba imesimamishwa na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika jana jioni .


Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 16 kabla ya Mbao FC kusawazisha kipindi cha pili dakika ya 46 kupitia kwa Habibu Kiyombo.

Simba walishambulia kwa kasi na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 49 kupitia kwa James Kotei. Mbao FC hawakukata tamaa na dakika ya 81 wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Boniphace Maganga na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare.

Huu ni mchezo wa kwanza raundi ya 4 ambao umewaacha Simba katika nafasi ya 2 wakiwa na alama 8 wakati Mbao FC wakisogea hadi nafasi ya 9 wakiwa na alama 4.

Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo huo,Simba haikuwa imeruhusu hata goli moja kutikisa wavu wake,rekodi ambayo sasa imefutika baada ya Mbao kutumbukiza kimiani goli mbili
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: