Kamati iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto ulioteketeza Soko la SIDO Jijini Mbeya imekabidhi ripoti yake leo ikionyesha chanzo cha moto huo kuwa ni jiko la Mkaa ndani ya kibanda cha mama lishe.
Ripoti hiyo imebaini kuwa hasara iliyosababishwa na moto huo ni zaidi ya Tshs Bilioni 14 kutokana na mali za wafanyabishara katika soko hilo kuunga zote.
Mkuu wa Mkoa Amos Makala atangaza eneo hilo rasmi kuwa Soko la kudumu,aagiza iwekwe miundombinu ya kudumu kwa kuzingatia tahadhari ya moto.



Post A Comment: