ads


KIKOSI cha Simba kimedhihirisha kuwa kina thamani ya bilioni moja baada ya kuonyesha uwezo wa juu kwa kuibuka na Ngao ya Jamii katika mechi ya ufunguzi rasmi wa pazi la Ligi Kuu Bara iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.


Katika mechi hiyo ambayo timu zote zilicheza kandanda la kuvutia, zilimaliza dakika 90 kwa sare tasa hivyo kuingia hatua ya matuta na Simba kushinda kwa penalti 5-4.

Kipindi cha kwanza

Dakika 45 za kipindi cha kwanza, Simba inayonolewa na Mcameroon Joseph Omog, ilifanya mashambulizi zaidi, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini kutumia vyema nafasi hizo walizotengeneza.

Dakika ya tano kipa mpya wa Yanga Youthi Rostand alidaka shuti la Ally Shomary aliyepokea pasi ya Haruna Niyonzima na kuikosesha Simba nafasi ya kufunga.

Aishi Manula, kipa mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Azam FC, aliwahi kupangua mpira wa kona uliopigwa na beki Juma Abdul na kuifanya Yanga ikose bao dakika mbili baadaye.

Dakika ya nane beki wa kati wa Yanga, Andrew Vicent "Dante" aliruka na kuokoa shuti lililopigwa na Emmanuel Okwi ambaye aliunganisha pasi safi ya Shiza Kichuya na kuokoa hatari hiyo langoni mwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Burundi Laudit Mavugo alipiga mpira nje kwa kichwa akiwa jirani na lango la Yanga na kupoteza nafasi nyingine kwa timu yake katika dakika ya 16 huku Okwi naye akipiga pembeni na kuharibu kazi nzuri iliyofanywa na Niyonzima katika dakika ya 18.

Yanga ilijibu mapigo kwa kufanya shambulizi, lakini mshambuliaji wake Emmanuel Martin alipiga shuti pembeni na kuharibu kazi ya kiungo Thabani Kamusoko dakika ya 24.

Manula alidaka kiufundi na kwa kujiamini shuti la Abdul katika dakika ya 40.

Kipindi cha pili

Simba ilianza kwa kasi, lakini Mavugo alipiga pembeni mpira wa kichwa na kupoteza nafasi ya kufunga katika dakika ya 46.

Kipa wa Yanga Rostand aliwahi kutoka katika eneo lake na kuokoa mpira ambao ulikuwa unafuatwa na Okwi aliyefanikiwa kumzidi mbio Abdul.

 Dakika ya 65 Yanga ilipoteza nafasi nyingine ya kufunga baada ya Manula kuwahi kudaka mpira uliopigwa na Ngoma ambaye alifanikiwa kumtoka beki wa Simba Method Mwanjali.


 Dakika 79 Manula alidaka tena shuti la Emmanuel Martin na kuwanyima Yanga nafasi ya kufunga.

SIMBA WATANGULIA, WAANZA SHANGWE

Saa 9:15 Kikosi cha Wachezaji wa Simba kiliwasili kwenye Uwanja wa Taifa na kwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo viko katika upande wa kulia wa uwanja.

Kwa kawaida vyumba hivyo hukaliwa na Yanga lakini kwa sababu mechi ya leo Yanga ndio mwenyeji, watakaa katika vyumba vya upande wa kushoto ambavyo hutumiwa zaidi na Simba anapokuwa mwenyeji katika mechi za zozote kwenye uwanja huo.

Saa 10:12 mabingwa hao wa Kombe la FA pia walikuwa wa kwanza tena kuingia uwanjani kupasha tayari kwa mchezo huo wa kuashiria ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18.

Katika kuonyesha hali ya kujiamini, mshabiki wa Simba walianza kushangilia kwa kusimama pamoja na kushangilia huku wakinyanyua mikono juu.

Hali hiyo iliwafanya mashabiki wa Yanga kutulia wasijue la kufanya na walishindwa kufanya chochote.

Simba ya kwanza uwanjani

Saa 9:15 Kikosi cha wachezaji wa Simba kiliwasili Uwanja wa Taifa na kwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo viko katika upande wa kulia wa uwanja.

Kwa kawaida vyumba hivyo hukaliwa na Yanga, lakini kwa sababu mechi ya leo Yanga ndio mwenyeji, watakaa katika vyumba vya upande wa kushoto ambavyo hutumiwa zaidi na Simba anapokuwa mwenyeji katika mechi za zozote kwenye uwanja huo.

Saa 10:12 mabingwa hao wa Kombe la FA pia walikuwa wa kwanza tena kuingia uwanjani kupasha.

Katika kuonyesha hali ya kujiamini, mashabiki wa Simba walianza kushangilia kwa kusimama pamoja na kushangilia huku wakinyanyua mikono juu.

Hali hiyo iliwafanya mashabiki wa Yanga kutulia wasijue la kufanya na walishindwa kufanya chochote.

Kamusoko aiongoza Yanga

Saa 9:35 mchana, Yanga waliingia uwanjani huku wachezaji wake wakiwa wanaongozwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Saa 10:22 kiungo Mzimbabwe wa timu hiyo Thabani Kamusoko aliongoza wachezaji wenzake kuingia uwanjani kuanza kupasha miili yao na kufuatiwa na waamuzi wa mchezo huo.

Yanga: Youthi Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Andrew Vicent "Dante", Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.

Simba: Aishi Manula, Ally Shomary, Erasto Nyoni, Salim Mbonde, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Laudit Mavugo

Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia jana aliwakabidhi wajumbe wa kamati ya utendaji kila mmoja mipira 100 ambayo ni maalum kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana katika kanda zao.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: