Rais Jacob Zuma ameliambia Bunge kwa maandishi kwamba hamiliki mali yoyote nje ya Afrika Kusini na wala hajawahi kuomba makazi kwa ajili yake wala familia yake ughaibuni.
Majibu hayo yanatokana na swali la Mbunge wa Cope, Willie Madisha aliyetaka kujua kama Zuma amewahi kuomba makazi au alinunua nyumba katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili yake au familia yake.
"Zaidi ya hayo, sijawahi kumuomba yeyote kununua nyumba kwa ajili yangu wala kwa niaba yangu ughaibuni. Nathibitisha kwamba sijawahi kuomba makazi yoyote nje ya Afrika Kusini, kwangu mwenyewe au familia yangu,” amesisitiza katika taarifa.
Post A Comment: