Serikali ya Tanzania imekanusha kuingilia masuala ya uchaguzi yanayoendelea huko nchini Kenya na kusema hawana mamlaka ya kuingilia chaguzi za nchi aina yoyote duniani.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Dr.Augustine Mahiga wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari leo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam na kusema Tanzania haina mpango huo kwa nchi yeyote na wala nchi hizo hazijawi kuingilia uchaguzi wa Tanzania.
"Hao wanaoingilia jambo hili na kuituhumu Tanzania kuhusu jambo hili waache mara moja kwa kuwa ni siasa za kuchafuana kama hizi hazina maslahi kwa wananchi wa nchi zote, hivyo tutachukua hatua za kisheria kwa wote watakaojihusisha na habari hizo ambazo hazina uhakika", amesema Dr. Mahiga.
Pamoja na hayo, Dr. Mahiga amewataka watu wanaofanya vitendo hivyo waache mara moja kabla sheria hazijachukua mkondo wake.
Post A Comment: