Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi cha Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kumpa hongera Rais John Pombe Magufuli kwa kuleta maendeleo katika nchi na jimbo lake na kusema mtu ambaye anapinga maendeleo si mtu mzuri.
Zitto Kabwe amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi wa Kigoma na kuwashukuru pia.
"Tunashukuru sana leo kwa uzinduzi wa mradi wa maji ambao utamaliza kabisa tatizo la maji katika mji wetu wa Kigoma. Licha ya kuwa tunatoka katika chama tofauti ila maendeleo hayana chama na hili Rais Magufuli umeonyesha njia kwani umekuja hapa Kigoma Mjini licha ya kuwa mji huu unaongozwa na upinzani. Kwa hiyo maendeleo hayana chama na asijitokeze mtu yoyote akafanya jitihada za kukwamisha mambo ya maendeleo mtu huyo atakuwa hana maana" alisisitiza Zitto Kabwe
Jiwe la msingi la mradi mkubwa wa Maji Manispaa ya Kigoma Ujiji litawekwa leo tarehe 22/07/2017 na Rais Magufuli na wananchi wa Kigoma watarajia kuanza kupata maji kuanzia Novemba 2017.
Post A Comment: