Rais Magufuli amewasili kwenye chanzo cha mradi mkubwa wa maji na amezindua mradi utakaozalisha lita 42 milioni kwa siku utakaomalizika Novemba 30, mwaka huu.
Amemsifu mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe kwa kushirikiana na serikali kuleta maendeleo akisem Zitto ni tofauti na wanasiasa wengine wa upinzani.
Pia ameahidi kushughulikia tatizo la wafanyakazi wa meli ya MV Liemba ambao inadaiwa wamekaa miezi 19 bila kulipwa mishahara.
Ameagiza Mkuu wa Mkoa Kigoma, Brigedia Jenerali, Mstaafu Emanuel Maganga kufuatilia idadi ya watumishi ambao hawajalipwa mishahara.
Post A Comment: