Mwigizaji John Heard aliyejizolea umaarufu kwa kuigiza kama baba katika filamu za Home Alone, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.
Mwili wake aligundulika na mhudumu wa hoteli aliyofikuwa amefikia kwa ajili ya mapumziko baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa mgongo jijini California, Marekani.
Heard alikuwa akiigiza kama Peter McCallister katika filamu za Home Alone akiwa baba wa Macaulay Culkin maarufu Kelvin.
Ameigiza katika filamu mbili kati ya hizo ambazo ni Home Alone na Home Alone 2: Lost in New York
Post A Comment: