ads

Rais John Magufuli amesema anapenda taasisi zinazohimiza maendeleo badala ya zile zinazohamasisha wanafunzi wazae kisha warudi shule.


Ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation. Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Manzana, Chato.

“Nazipenda taasisi zinazohimiza maendeleo si zinazotaka watu wazae halafu warudi shuleni. Mmekalia kusema kuwa watu wazae halafu warudi shule, sasa si watazaa kila mahali, darasa lote litakuwa na mimba,” amesema.

Amezitaka taasisi nyingine ziige mfano wa taasisi ya Mzee Mkapa, na kusema ni vyema kusimama majukwaani na kutangaza vitu vyenye maendeleo.

“Vipo vitu ‘tangible’, taasisi zipo kwenye majukwaa, wanaletewa hela nyingi, lakini ‘impact’ hakuna nani aliyewaambia kuwa kila anayepata mimba amebakwa?” Amehoji na kuongeza:

“Hata kwangu kuna watu wanaozaa na wala hawajabakwa, hata mtoto wa mdogo wangu alizaa bila kubakwa, alipoulizwa imekuwaje (anaongea kwa lugha ya kisukuma) akanizalia mtoto akamuita John, akakaa kidogo akazaa tena mtoto akamwita Samia.” Amesema na kusababisha kicheko kwa umati huo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: