Rais John Pombe Magufuli leo Julai 23 atafanya ziara ya siku mbili mkoani hapa kwa ajili ya uzinduzi wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema Rais Magufuli atawasili mkoani Tabora akitokea Kigoma ambapo wanatarajia kumpokea katika Wilaya ya Kaliua.
Amesema kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Kaliua atazindua barabara kutoka Kaliua hadi Kazilambwa na baadaye atapata fursa ya kuwahutubia wananchi.
Mwanri amesema akiwa njiani kuelekea Tabora Rais Magufuli atazinduza barabara ya Urambo hadi Tabora siku hiyo hiyo na atawahutubia wakazi wa Urambo na kisha kuelekea Tabora.
Amesema kesho Jumatatu Rais ataweka Jiwe la Msingi ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuja katika miji ya Nzega , Igunga na Tabora na baadaye kuzindua upanuzi na ukarabati wa njia za kurikia Ndege katika Uwanja wa Tabora.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ameongeza kuwa siku hiyo hiyo ,Rais atazindua barabara ya Tabora hadi Nzega na ile ya Tabora hadi Nyahua na mchana atawahutubia wakazi wa Tabora katika Viwanja vya Chipukizi.
Alisema ujio wa Rais Magufuli kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora ni sawa na usemi usemao Mgeni Njoo Mwenyeji Apone kwani zara yake mkoani hapa inazidisha matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na jirani zake ya kuendelea kufunguka milango au fursa mbalimbali za uchumi baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya miundo mbinu.
Post A Comment: