David Beckham anaonekana kuwachanganya baadhi ya watu kwa kitendo chake cha kupost picha mitandaoni bila kutaja kama yupo katika moja ya mbuga hapa nchini Tanzania.


Beckham alitua nchini kimya kimya wikiendi iliyopita majira ya usiku akiwa ameongozana na familia yake na kuelekea mahali pasipo julikana huku baadhi ya wadau wakidai alikuwa ameelekea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.

Kitendo hiko kimewafanya watu kumshambulia kwenye kila picha aliyopost mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza.

Hata baadhi ya mastaa wa Bongo wameonekana kushangazwa na kitendo hicho huku wengine wakitoa yao ya moyoni kupitia mtandao wa Twitter, kati yao ni Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Mwasiti. “Mbona hatoi Taarifa kwa wenye nchi Yetu🤣🤣🤣🤣atajuta nipe username yake kwanza 🤣🤣🤣🤣hata simfologi,” ameandika Lulu.

Naye Mwasiti ameandika, “😂😂 huyu beckham huyu..sasa sisi ni mwendo wa kuweka bendera yetu 🇹🇿🇹🇿 tu kwenye kila picha yake mbugani kagoma kusema alipo 😂😂@OfficialLizyM.”

Hata hivyo Fid Q amewachana watu wanaolalamikia tukio hilo, “Nimekuta watu wananung’unika juu ya suala zima la ujio wa DEVI mbugani kwetu eti kwasababu kila akipost hasemi kama yupo TZ..Mlimfadhili? 😀.”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: