Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.
Sirro ameyasema hayo jana (Jumamosi) katika ziara yake ya kwanza mkoani Morogoro tangu ateuliwe kuwa IGP na kusisitiza kuwa polisi wanafanya kazi usiku kucha kudumisha hali ya usalama.
“Hatulali, tunafanya kazi kwa juhudi kubwa, lakini ni lazima wananchi watupe ushirikiano na nyinyi waandishi wa habari pia mnatakiwa mwandike kwa hekima bila uchochezi,” amesema.
Sirro amesema amefanya ziara hiyo Morogoro na katika maeneo mengine nchini ili kuzungumza na polisi namna ya kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Post A Comment: