ads

Mwanamuziki nyota na tajiri nchini Marekani, Beyonce Knowles amejifungua watoto mapacha.


Chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na familia ya mwanamuziki huyo, kimelieleza Shirika la Habari la CCN, leo.

 Taarifa ya kuzaliwa kwa mapacha hao imerushwa katika magazeti ya mitandao jioni hii.

Kadhalika, Gazeti la US Weekly limethibitisha kuwa Beyonce amejifungua lakini halikutaja jinsi na tarehe waliyozaliwa mapacha hao.

 Beyonce ambaye ni mke wa mwanamuziki Jay Z, aliutangaza ujauzito wake Februari mwaka huu, katika ukurasa wake wa Instagram.

Beyonce na Jay Z wana mtoto mwingine wa kike, Blu Ivy mwenye miaka mitano
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: