ads

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis ametaka mjadala wa kimataifa uandaliwe wa kususluhisha mvutano unaozidi kutokota kati ya Marekani na Korea kaskazini akisema kwamba swala hilo limekuwa kaa la moto.


Papa Francis amewaambia wanahabari kwamba mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi.

Awali manowari ya kivita ya Marekani iliwasili karibu na rasi ya Korea, saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora ambalo lilitibuka.

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumua Korea Kaskazini kwa kuiokosea heshima jirani wake China na rais wake.

Hivi majuzi Trump alimulika rais wa China Xi Jinping na kumpongeza kwa kujitahidi kutatua mzozo wa Korea Kaskazini.

Jaribo la kombora la Korea Kaskazini lilijiri saa chache baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: