ads

Baada ya Ben Pol kuchafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Alhamisi ya wiki iliyopita kutokana na picha zake zinazomuonyesha akiwa nusu mtupu kuenea mitandaoni na kumsababishia kukutana na mvua kubwa ya matusi, msanii huyo amefunguka sababu ya kufanya hivyo.


Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Tatu’, ameisema Junanne hii kuwa alifanya hivyo ili kuendana na kasi ya biashara ya muziki ambayo amedai kwa sasa inahitaji matangazo.

“Ile picha unajua muziki umebadilika na unataka kufanya promotion ya kitu chako unatakiwa kutoa material zote ya project yako. Sasa mimi nilikuwa anatoa wimbo ambao unazungumzia ufungwa, mtu ambaye hana uhuru, hawezi kusema,” alisema BenPol. “Kwahiyo mimi nimefanya hivyo ili kuwakilisha kile kitu ambacho nimekifanya ndani ya wimbo, sikuona kama nina sababu na kufanya kitu tofauti wakati kuna njia moja ya kupita ili kufanikishha jambo langu,”

Hata hivyo muimbaji huyo amedai hakufanya vile ili kutafuta kiki kama baadhi ya watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: