ads

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa bei ya unga wa ugali kwa sasa ipo juu kuliko hata bei ya mafuta ya magari jambo ambalo linafanya wananchi kuumia zaidi na ugumu wa maisha.


Zito Kabwe amesema kwa sasa Bei ya Unga wa Sembe 1kg ni  Shilingi 2,300/= huku Mafuta ya Petroli lita moja ikiuzwa kwa Shilingi 2,060/= huku akishangaa kuwa ni mara yake ya kwanza kuona Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari.

“Bei ya Unga wa Sembe 1kg TZS 2,300/= ( wastani ). Bei ya Mafuta ya Petroli 1lita TZS 2,060/= ( wastani). Kwa mara ya kwanza Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari“Ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook huku akiendelea kuhoji ukimya wa Serikali juu ya mfumko huo wa Bei

“Gharama hizi za maisha Kwa wananchi ni kubwa mno, hazistahmiliki na zinaingiza raia wengi kwenye umasikini. Serikali ipo kimya kana kwamba kila kitu kipo sawa“Ameandika Zitto Kabwe.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: