Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku amekutana na nahodha wa Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta huko Ubelgiji alikoenda kwa ajili ya Mkutano wa kutatua migogoro ya kisiasa nchini Libya.


Mzee Kikwete mapema baada ya kukutana na nyota huyo anayekipiga kunako Klabu ya Genk alionesha furaha yake na kuandika ujumbe mzuri wa kufurahishwa kwa kukutana nae.

“Nikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetu @samatta77 leo hii“, Ameandika Kikwete lwenye ukurasa wake wa Twitter.

Samatta nae hakuchukulia poa shavu hilo la kutembelewa na Rais Mstaafu kwa Kuandika “Ni wakati mzuri siku zote kukutana na our former president Mr @JakayaKikwete Wise and charming man. Asante sana mheshimiwa mungu akuweke” .

Mbwana Samatta ni moja ya wachezaji ambao wametajwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kuvaana na Lesotho mwezi ujao kwenye mechi za kufuzu AFCON.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: