ads

Vikosi vya Usalama nchini Kenya viko katika hali ya ulinzi mkali na tahadhari baada ya kupokea taarifa za ujasusi kwamba wanamgambo wamekuwa wakipanga mashambulizi ya kigaidi wakati au baada ya sikukuu ya Pasaka.


Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, George Kinoti ambapo ameeleza kuwa wamepokea taarifa za ujasusi zikieleza kuwa wanamgambo tisa wanapanga mashambulizi, hivyo tayari vikosi vya usalama vimejiimarisha na kuhakikisha kunakuwa na tahadhari ya juu kudhibiti mashambulizi yasitokee.

Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi wote kuwa waangalifu kwa hali ya juu kabla ya sikukuu ya Pasaka na kuripoti shughuli zote watakazozitiliwa shaka.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: