Maafisa wa polisi wa Tanzania wamewaua watu wanne wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya maafisa wanane wa polisi katika usiki wa Alhamisi kusini mwa mji wa Dar es Salaam.
Kamishna wa polisi anayehusika na uchunguzi Nsato Mssanzya amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba wanne hao walipigwa risasi muda mfupi Ijumaa alfajiri wakati wa msako.
Maafisa waliouawa waliripotiwa kushambuliwa walipokuwa wakipiga doria katika mji huo.
Kamishna huyo alisema kuwa bunduki nne zimepatikana kutoka kwa washukiwa waliouawa ikiwemo bunduki mbili zilizoibwa kutoka kwa polisi waliouawa, huku operesheni ya kuwasaka washukiwa waliosalia ikiendelea.
Inspekta jenerali wa polisi Ernest Mangu alianzisha uchunguzi siku ya Alhamisi usiku.
Tayari rais Magufuli ameshutumu mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanywa.
Post A Comment: