ads

Beki wa Simba Abdi Banda hivi sasa yupo huru kuitumikia klabu yake ya Simba baada ya leo adhabu yake kutangazwa  kumaliza kutumikia adhabu yake . Mchezaji huyo alifungiwa na Bodi ya Ligi baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar,  George Kavila


Kamati ya nidhamu ilikaa siku ya jana na wakati inakaa tayari mchezaji huyo alikuwa amekosa mechi mbili hivyo kamati ilipitia  na kusikiliza pande zote mbili na kufanya maamuzi kuwa zile mechi mbili ambazo mchezaji huyo alizikosa ndiyo adhabu yake tosha kwa kosa alilofanya.

Awali mchezaji huyo baada ya kufanya tukio hilo ambalo mwamuzi hakuliona, alisimamishwa kucheza ligi kuu kusubiri maamuzi, na akakosa michezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.

Mchezaji huyo wa Simba ataungana na wachezaji wengine wa klabu hiyo ambao wataingia kambini siku ya Jumapili kujiweka sawa dhidi ya mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu Bara ambazo zinaendelea nchini. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: