Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima amewataka wananchi
wasikubali kumpa kadi ya kupigia kura mtu yeyote isipokuwa kuionyesha
kwenye kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi.
Sambamba
na hilo, Kailima amewaambia waandishi wa habari kuwa ACT-Wazalendo na
vyama vingine vya siasa vyenye wagombea katika uchaguzi mdogo wa
madiwani na ubunge, kutumia haki zao kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji
wa maadili kwa kamati husika.
“Kwa
kuzingatia sehemu ya 5.4 ya maadili ya uchaguzi, Tume inavikumbusha
vyama vya siasa kuwasilisha malalamiko yao katika kamati ya maadili
ngazi ya kata ndani ya saa 72 tangu kutokea kwa ukiukwaji wa
maadili,”amesema Kailima.
Amesema
kama chama hakitaridhika na uamuzi utakaotolewa na kamati ya maadili
ngazi ya kata, kwa kuzingatia sehemu ya 5.7(a) ya maadili ya uchaguzi
awasilishe rufaa kwa msimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ndani ya saa
24 tangu uamuzi wa ngazi ya kamati ya kata kutolewa.
Kailima
amesema endapo chama bado hakijaridhika na uamuzi ya ngazi ya jimbo,
kwa kuzingatia sehemu ya 5.7(b) na (c), kina fursa ya kuwasilisha rufaa
kamati ya maadili ya ngazi ya taifa au ngazi ya rufaa ambayo ni NEC.
“Kwa
mujibu sehemu ya 5.7(e) ya maadili ya uchaguzi, kama chama au mgombea
hakuridhika na uamuzi ya kamati ya rufaa atakuwa na fursa ya kuwasilisha
malalamiko yake mahakamani baada ya uchaguzi kufanyika kwa mujibu wa
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya
Serikali za Mitaa, Sura ya 292,” alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: