ads

KATIKA kuonyesha kuwa Siasa si uadui na kuna maisha maada ya siasa,Leo hii katika ibada ya kuaga mwili wa mpiga picha wa Tanzania Daima Joseph Senga,makada maarufu wa CCM na Chadema Edward Lowassa ,Nape Nnauye na Freeman Mbowe wameshirikiana katika tukio hilo.


Makada hao ambao leo hii wamekubali kuweka tofauti zao pembeni na kuamua kushirikia katika tukio hilo muhimu la kuomboleza msiba huo wameonekana wakiwa pamoja na kuketi katika viti vya karibu hali iliyoashiria kuwa Siasa si ugomvi.


Itakumbukwa kuwa Nape Nnauye kwa nyakati tofauti alikuwa akiongea kashfa juu ya Lowassa na Chadema,huku Mbowe naye kwa nyakati tofauti akinukuliwa akiongea kashfa dhidi ya CCM na Nape


Swahiba media inakusogezea picha ya tukio hilo na jinsi ilivyokuwa ,huku akiwataka watanzania kudumisha umoja wetu na kutokubali kugawanywa au kutenganiswa na wanasiasa ambao wenyewe wanakutana na kuelewana huku sisi tukiendeleza uhasama usio na tija kwa mustakabali wa maisha yetu na amani ya nchi yetu 


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: