Bondia maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, Jana ametangaza rasmi
kustaafu mchezo wa masumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa
ma-promota pamoja na kutopata faida katika mchezo huo.
Cheka ambaye anakabiliwa na tuhuma za
kuchukua pesa na kugoma kupanda ulingoni katika pambano lililokuwa
limeandaliwa siku ya Krismasi, amesema amechoshwa na kile alichokiita
kuwa ni utapeli wa mapromota, na kwamba sasa atajikita zaidi katika
mapambano ya kuhamasisha vijana.
Akiwa amedumu kwenye ndondi nchini kwa
takribani miaka 19, Cheka amesema mchezo huo umetawaliwa na majungu, na
fitina huku watu wengi wakifikiri kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna
anachokipata zaidi ya umaarufu na kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.
"Huu mchezo una majungu na fitina,
hakuna faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na waandishi wa habari, hakuna
pesa, tunapata pesa gani, watu wanadhani tunapata pesa, nitabaki
kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha vijana katika ngumi pamoja na
kufanya biashara nyingine nipate pesa, nimedumu kwenye ngumi zaidi ya
miaka 19, nimevumilia mengi" Amesema Cheka.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI


Post A Comment: