UPELELEZI wa kesi mbili zinazomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa
Kampuni ya Jamii Media Limited, Mexence Melo (40), haujakamilika.
Kesi hizo zimetajwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba na Hakimu Mkazi, Geofrey
Mwambapa.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mohammed Salum alidai kuwa kesi hiyo
imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake haujakamilika
hivyo, aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Simba ambaye anasikiliza kesi namba 456
na Hakimu Mwambapa anayesikiliza kesi namba 457, waliahirisha kesi hiyo
hadi Januari 26, 2017 na kutaka upande wa mashitaka kuhakikisha
upelelezi huo unakamilika haraka.
Inadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi mwaka huu na Desemba 13, mwaka huu
maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, mshitakiwa akiwa Mkurugenzi wa
kampuni hiyo inayoendesha tovuti ya Jamii Forum, alishindwa kutoa
taarifa kuhusu miliki hiyo huku akijua kwamba jeshi hilo linafanya
uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyochapishwa kielektroniki kwenye tovuti
hiyo.
Pia inadaiwa mshitakiwa alizuia jeshi hilo kufanya uchunguzi kinyume
na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka
2015.
Salum alidai kuwa kati ya Mei 10 mwaka huu na Desemba 13 mwaka huu
maeneo ya Mikocheni, akiwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, alilizuia jeshi
hilo kufanya uchunguzi kwa kushindwa kutoa taarifa zilizochapishwa na
tovuti hiyo.
Aidha, katika kesi ya tatu, mshitakiwa alikabiliwa na mashitaka
mawili ikiwemo la kuendesha mtandao kwa usajili usio wa Tanzania na
kuzuia jeshi kufanya uchunguzi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: