Msemaji wa klabu ya Simba Haji
Manara ameamua kuwa muungwana kwa kumuombea msamaha kwa Rais wa
TFF,Jamal Malinzi msemaji wa Yanga Jerry Muro ambaye amefungiwa mwaka
mmoja kujihusisha na soka nchini Tanzania.
Kwako Rais wa TFF
Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi
kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na
upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka
nchini,
kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.
Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha
mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na
mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari
ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,

Ninajua kwa kufanya hivyo
atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi
wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,
Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili
mimi binafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia
kutorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa
dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao
wanasimba,
Tunamiss rikaka zake
zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. kwangu Mh Rais nina hakika
utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati
zilizomfungia kumuachia huru,
ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.
Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka. Wako
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: