Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania UWT,ya Chama cha Mapinduzi CCM
-katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imelazimika kumjengea nyumba Bibi
Rukia Salehe mwenye umri wa miaka zaidi ya 75 ambaye amekuwa akilala nje
kwa miaka minne mfululizo licha ya juhudi zake za kuomba msaada kwa
mamlaka husika kushindikana.
Akizungumza kwa masikitiko bibi rukia salehe anasema nyumba
aliyokuwa akiishi hapo awali ilianguka baada ya kuwa na nyufa
nyingi,hivyo kukosa uwezo wa kujenga nyumba nyingine,huku akisisitiza
katika maisha yake hajawai kupata mtoto licha ya kutumia muda mwingi
kulea watoto wa ndugu na marafiki lakini wameshindwa kumsaidia.
Akimzungumzia bibi huyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Matopeni
Omar Hussein anasema licha ya bibi huyo kuomba msaada ofisi ya mkuu wa
wilaya lakini amegonga mwamba,hali iliyolazimu diwani wa Chama cha
Mapinduzi kwa kushirikiana na wanachama wa UWT kumsaidia ili kumuondoa
katika mazingira hatarishi.
Kibanda cha bibi Rukia anachoishi ni hatarishi lakini amekuwa
akikitumia kulala kuhifadhi vitu vyake na kupikia huku mvua jua
likimuwakia kutwa kucha.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: