AZAM imeingia mkataba wa miaka mitatu na kocha wake wa zamani Kalimangonga ‘Kally’ Ongala kuifundisha timu hiyo.
Timu hiyo imefikia hatua hiyo baada ya kutimua benchi lote la ufundi
likiongozwa na Zeben Hernandez Rodriguez. Habari za uhakika kutoka Azam
zilisema jana tayari Kally yupo Dar es Salaam na kuna masuala madogo
yanakamilishwa.
Kally, aliyekuwa msaidizi wa Stewart Hall Azam, kwa sasa ni kocha wa Majimaji aliyokuwa na mkataba nao wa mwaka mmoja.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba hakutaka kulizungumzia hilo jana
lakini Mwenyekiti wa Majimaji Humphrey Milanzi alisema wapo kwenye
mazungumzo na viongozi wa Azam juu ya kuvunja mkataba huo wa mwaka
mmoja.
“Ni kweli viongozi wa Azam walitupigia simu kuhusu kumtaka Kally na
sasa tunaangalia namna ya kuvunja mkataba wa mwaka mmoja tulioingia kati
yetu na kocha Kally,” alisema.
Mapema jana Kawema aliwaambia waandishi wa habari kwamba timu yao
itakuwa chini ya kocha wa vijana Iddi Nassor ‘Cheche’ kwa muda
akisaidiwa na Iddi Abubakar.
Jopo la makocha hao wa Hispania, mbali na Hernandez wengine ni Yeray
Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na
Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez.
Kawemba alisema uamuzi wa kuwaondoa makocha hao umefikiwa na Bodi ya
Wakurugenzi wa timu hiyo juzi, na umetokana na mwenendo mbaya wa Azam FC
kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo imefikia raundi ya
pili hivi sasa.
“Tunawashukuru kwa mchango wao, walitupa taji la ngao ya jamii
tuliweza kuifunga Yanga kwa penalti 4-1 tunawatakia maisha mema huko
waendako,” alisema.
SOURCE - Habari Leo
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: