MAMBO magumu. Hatua mbalimbali
zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa kila mtu
anajiingizia mapato kutokana na shughuli halali na si kutegemea ‘dili’
za mjini zimeendelea kuibua vilio kutokana na ukata mkali kwa mamia ya
watu.
Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa, umebaini kuwa
miongoni mwa waathirika wakubwa wa uhaba huo wa fedha zilizokuwa
zikipatikana kirahisi kupitia ‘dili’ nyingi, zilizokuwapo walau mwaka
jana kulinganisha na sasa, ni pamoja na wajasiriamali mbalimbali ambao
sasa wamejikuta wakiwa katika hali mbaya kiuchumi.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, umebaini kuwa baadhi ya wajasiriamali
wamejikuta wakifilisika baada ya biashara zao kuyumba na mwishowe
kushindwa kulipa mikopo waliyoipata kutoka benki na taasisi zingine za
fedha.
Hatua hiyo imesababisha kutwaliwa mali walizoziweka dhamana, zikiwamo
viwanja, majengo kama ya shule na nyumba za makazi, nyumba za kulala
wageni, hoteli pia magari.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: