WAFANYABIASHARA wakubwa wa Mkoa wa Arusha wamepongeza kazi nzuri
iliyofanywa na Rais John Magufuli katika mwaka wake mmoja madarakani,
ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kudhibiti matumizi ya fedha ya umma na
kurejesha uadilifu na uwajibikaji katika kazi.
Waliyasema hayo jana katika mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo mjini hapa.
Alikutana nao kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za kila siku.
Mfanyabiashara Nicholaus Duhia, alisema Rais Magufuli amesimamia vema
ulipaji kodi, kurudisha heshima ya uadilifu serikalini na kupiga vita
ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma zilizokuwa zikitumika
kiholela bila ya kuwa na utaratibu maalumu.
Duhia ambaye ni wakili, mkaguzi wa hesabu na ushauri wa kodi wa
kampuni ya Tax Plan Associates ya Arusha, alisema hakuna anayeweza
kubisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema na kutoa ombi kupitia kwa Gambo kuwa Rais Magufuli katika
mwaka wa pili wa uongozi wake anapaswa kurudisha imani na amani kwa
wafanyabiashara nchini ili wafanye kazi bila woga.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa A Lodhia Group Enterprises, Sailesh
Pandit, alisema mbali ya kumkubali Rais Magufuli kwa utendaji kazi wake
wa falsafa ya Hapa Kazi Tu, amesema anakunwa pia kwa jinsi heshima ya
kazi ilivyorejea serikalini, huku watendaji wa serikali wakichapa kazi
kwa weledi.
Wafanyabiashara Willibrod Chambulu wa Kibo Safaris na Atul Nittal wa
Mount Meru Millers wameiomba serikali iangalie namna ya kupunguza
utitiri wa kodi. Gambo aliwahakikishia kuwa serikali itakuwa imara na
kuwalinda na kuwasaidia watakapokwama, lengo likiwa kuwataka wafanye
kazi kwa ufanisi, bila ya kipingamizi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: