ads

Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema ameibuka  katika mkutano wa na Rais John Magufuli uliofanyika mjini Kahama.


Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi CCM akisema kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza mkia, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.

Hivi karibuni akihutubia mkutano Mkuu wa CCM, Rais Magufuli akizungumzia waliotoka kwenye chama na kurejea tena, alitoa mfano wa ng’ombe aliyekatwa mkia, akisema huwezi kumzuia kurejea zizini lakini wenzake wanamkua kuwa hana mkia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli amesema amekwenda kwenye mkutano huo kwa kuwa kazi anayoifanya Rais Magufuli ndiyo ambayo alikuwa anapigania wakati akiwa mbunge kwa kuwa Shinyanga rushwa ilikuwa imekithiri.

Amesema na hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho akisafishe.

"Kubadilisha msikiti siyo kuacha Uislamu, nyumba itaposafishika nitarudi," amesema Lembeli. 


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: