Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania TPA imetangaza kuanza kufanya
maboresho ya bandari ya Dar es salaam ili kuondokana na msongamano wa
mizigo pamoja na kurahisisha upakuaji wa mizigo unayopitia katika
bandari hiyo.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi
Aloyce Matey amesema kumekuwa na ongezeko la mizigo inayopitia katika
bandari hiyo kwa miaka mitano mfululizo hali inayowalazimu kufanya
marekebisho makubwa ili kuendelea kutoa fursa kwa nchi jirani kuendelea
kutipisha mizigo katika Bandari ya Tanzania.
Mhandisi Matey amesema bandari ya Dar es salaam inakabiliwa na uchakavu wa Miundombinu na kuwa na kina kifupi cha maji cha mita 9 na ufinyu wa lango la kuingilia meli lenye upana wa mita 140 ambalo linaruhusu meli zenye urefu usiozidi mita 243 tu kuingia na meli kubwa zaidi zinashindwa kuingia.
Kwa Upande Mwingine,Msimamiz wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Marry Myaya amesema bandari ya Dar es salaam imefunga vifaa vya kupimia mafuta yanayopakuliwa katika Bandari hiyo kabla ya kufikishwa katika maghala

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: