ads

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa serikali yake imepigwa na butwaa na matamshi ya kushtua na ya aibu ya waziri mkuu wa Uingereza Bw David Cameron yakwamba Nigeria na Afghanistan ndio mataifa fisadi zaidi duniani.


Rais Buhari ameyasema hayo muda mchache tu baada ya kupata habari hiyo kumhusu waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.

Rais Buhari akizungumza kupitia msemaji wake, Garba Shehu ametaja matamshi ya Cameron kuwa ya aibu na kushtua.

”Kiongozi huyo wa Nigeria anasema labda Cameron alikuwa akizungumzia utawala uliondoka madarakani mwezi Mei mwaka uliopita wa aliyekuwa rais Goodluck Jonathan.

”Buhari alichaguliwa kwa jukwaa la kupamabana na ufisadi.”

”yeye ndiye kifagio cha ufisadi nchini Nigeria.”

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: