SERIKALI ya Korea imepanga kuleta nchini walimu wa masomo ya hisabati
na sayansi kwa shule za sekondari, kusaidia kupunguza uhaba wa walimu
wa masomo hayo. Itatekeleza azma hiyo kupitia Mpango wake wa Kusambaza
Walimu wa Kikorea katika nchi Zinazoendelea (KTDP).
Akizungumza jana alipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais wa
Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (NIIED), Kim Kwangho, alisema nchi yake
imekuwa ikisambaza walimu. Alisema mpaka sasa wamesambaza walimu 61
katika nchi mbalimbali zinazoendelea; na mwaka huu watasambaza walimu
140 kwa nchi 15.
“Tumeona katika kuunga mkono juhudi za serikali kuongeza walimu wa
masomo ya sayansi na kwa mara ya kwanza mwaka huu taasisi yetu
itasambaza walimu 10 hapa Tanzania kati yao watano watahusika katika
masomo ya hisabati na wengine watano watahusika na masomo ya Sayansi,”
alisema Kwang-ho.
Aidha alisema licha ya kusambaza walimu hao, Serikali ya Korea inatoa
ufadhili kwa wanafunzi wenye vipaji kimataifa ili kuendeleza masomo yao
katika taasisi za elimu ya juu nchini kwao, lengo likiwa ni kusaidia
kukuza viongozi wa baadae wenye elimu.
Kwang-ho alisema waombaji wa ufadhili huo ni wale waliosoma tu
Shahada ya kwanza na shahada ya Uzamili nchini; na haitawahusu wale wote
ambao wamewahi kusoma Korea.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: