ads

Kutangaza hapa piga : +255 759 202 132

MOYO wangu umegandwa na mavumbi, macho yamepofuka kwa machozi, kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani, kila mtu ananihukumu kwa uongo na hadithi za kutunga juu ya ndoa yangu pasipo kujua ukweli,” ndivyo anavyoanza kusimulia staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ akielezea wakati mgumu anaokutana nao baada ya kuwepo na mgogoro kwenye ndoa yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu hivi karibuni, msanii huyo alisema kila mahali anapopita ananyooshewa vidole kwa watu kumhukumu kuwa ni mkorofi kwenye ndoa yake jambo ambalo halina ukweli.
Akaeleza kuwa, siri za ndoa huzijua wahusika na kwamba hata yeye kufikia hatua ya kutengana na mumewe anajua chanzo ni nini na si rahisi kumueleza hata mama yake mzazi, ila watu wanatumia maneno makali yanayomuumiza.
“Kila mtu anasema analolijua, hakuna aliyenilazimisha kuolewa, kilichonifarakanisha na mume wangu tunakijua sisi wawili (yeye na mumewe), labda na watu wangu wa karibu, lakini kwa sasa maneno yamekuwa mengi sana, tena yenye kuumiza kiasi kwamba kuna wakati natamani hata kujitoa uhai.
“Vitu vingine ni vya ndani sana hata mama yangu mzazi siwezi kumwambia, ila maneno yamenizidia, haya, huyo Mike wanayemsema natoka naye, jamani nimemjua Mike kabla ya mume wangu, ilikuwaje nisitoke naye zamani ije kuwa leo? Naumia miye jamani, Mungu anajua, ipo siku kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Davina kwa sauti ya uchungu.
Chanzo: GPL
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: