ads
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015.
 
Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.
 
Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau gan
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: