ads
Klabu simba imesema haioni sababu ya kutonyakua kombe la ligi kuu tanzania bara kutokana na kujiimarisha kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu

Afisa habari wa simba sc, Haji Manara amesema "tunavijana ambao msimu uliopita hawakufanya vizuri ambapo kwa msimu ujao watafanya vizuri kwasabau wameshajiandaa vya kutosha na wamekomaa ambao wataungana na wachezaji wazoefu ili kukiimarisha zaidi kikosi hicho.

manara amesema usajili wa safari hii umeiweka timu sawa kwaajili ya kuchukua ubingwa kwani tumejipanga kila eneo ndani na nje ya uwanja

kwa upande wa usajili klabu hiyo imefanikiwa kumsajili raia wa uganda Hamisi Kiiza Diego mkataba wa miaka miwili kwaajili ya kuitumikia katika mechi za msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: