ads

MWANAMKE mmoja (25), mkaazi wa Pandani, amelazwa hospitali ya Wete Pemba, baada ya kumwagiwa maji moto na kijana Mfaki Ali Hamad, baada ya kukataa kufanya nae mapenzi kwa muda mrefu sasa.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinaeleza kuwa, kijana huyo alikuwa akimfuata kwa muda mrefu mwanamke huyo aliekwenye ndoa, akitaka kufanya nae mapenzi, bila ya mafanikio na kumuahidi kumfanyia lolote.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa, kijana Mfaki baada ya kukataliwa na mwanamke huyo, ndipo alipotimiza ahadi yake juzi usiku ya kumfanyishia kwa kumwagia maji moto, na kumsababisha mauimivu makali mwilini mwake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Sheihan Mohamed Shein alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema lilitokea majira ya saa 5:00 usiku, wakati mwanamke huyo alipokuwa chooni akijisaidia.

Alisema kijana huyo, aliitumia fursa ya mwanamke huyo kwenda kujisaidia usiku huo na kufanikiwa kumwagia maji moto alioyachanganya na rangi rangi, ambapo ilionekana mithili ya tindikali.

Kamanda huyo wa Polisi alisema, baada ya kutokea tukio hilo mwanamke huyo alifikishwa hospitali kwa matibabu, ambapo walikuwa na wasi wasi kwamba huwenda ni sumu aina tindikali.

“Daktari wa zamu wa hospitali ya Wete, alithitbitisha kuwa, hayo ni maji moto na sio tindikali kama watu waliovyoeneza taarifa’’,alifafanua Kamanda huyo.

Alieleza kuwa kwa mujibu wa daktari huyo, mwanamke huyo aliepatwa na ajali hiyo, amepata mivimbe sehemu mbali mbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na mgongoni na mapajani, ingawa hali yake inaendelea vyema.

Aidha Kamanda huyo alisema kijana huyo, alietenda kosa hilo anaendelea kusakwa na jeshi lake na atakapokamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ingawa taarifa za mwisho zinaeleza kuwa, tayari kijana huyo ameshatiwa mkononi na Jeshi la Polisi, ambapo hili ni tukio la kwanza kwa karibu miaka mitano ya karibuni kwa mwanamke kumwagia maji moto kwa sababu ya kimapenzi.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: