ads

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.


Akizungumza na  gazeti la Mwananchi , Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

“Namvulia kofia kabisa, huyu ni Rais  msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”

Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.

“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”

“Nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao wanatakiwa kutoka,”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: