
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
HATIMAYE nyumba za kifahari za Lugumi Enterprises zinatarajiwa kupigwa tena mnada Novemba 24 ikiwa wiki mbili baada ya kuvurugika ule wa awali uliofanyika Novemba 9, mwaka huu.
Wakati hilo likifahamika, katika kuonyesha kuwa bado ana ndoto ya kuzitwaa nyumba hizo, Dk. Louis Shika aliyeshinda mnada wa awali na kubainika baadaye kuwa hana fedha ya kuzilipia, amesisitiza kuwa anajipanga kivingine kwa kuzilipia zote huku akishuhudiwa na vyombo vya habari.
Nyumba hizo za Lugumi, ni mbili zilizoko eneo la Mbweni na nyingine iliyoko Upanga, zote zikipigwa mnada ili kufidia kodi ya mapato ambayo Lugumi inadaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).
Wiki iliyopita, mnada kwa ajili ya nyumba hizo ulivurugika baada ya aliyeibuka mshindi wa kununua nyumba zote tatu, Dk. Shika, kubainika kuwa hakuwa hata na senti tano ya kuzilipia. Baada ya hapo, mshindi huyo aliyeahidi kulipa Sh. bilioni 3.3 kwa ajili ya nyumba zote, aliishia mikononi mwa Polisi.
Tangu kujiri kwa tukio hilo, Dk. Shika amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kauli yake ya ‘Nadhani 900 itapendeza zaidi’. Hadi sasa, Dk. Shika amekuwa akiripoti polisi kila uchao wakati jeshi hilo likiendelea kumchunguza kutokana na kitendo chake kuharibu mnada wa Novemba 9, hasa baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya malipo ya awali kama masharti ya mnada yanavyotaka.
Awali, picha kadhaa kwenye mitandao zilimwonyesha Dk. Shika akipepewa na kuimbiwa nyimbo za kumpamba baada ya ushindi wake, hali ambayo baadaye iligeuka na kuibua gumzo baada ya kubainika kuwa hakuwa na fedha hizo na kwamba, hata sasa anaishi kwenye chumba kimoja tu cha kupanga, Tabata jijini Dar es Salaam.
Wakati wa mnada alioshinda, kuna mtu mmoja alijitokeza kununua nyumba mojawapo kwa Sh. milioni 700 na baadaye kupanda hadi milioni 750, lakini Dk. Shika akamshinda kwa kutaja Sh. milioni 800, mwingine akajitokeza na kutaja Sh. milioni 810, lakini Dk. Shika akamshinda na huyo pia kwa kauli yake maarufu hivi sasa ya:‘900 itapendeza zaidi’.
Katika taarifa yake, dalalali wa mnada wa nyumba hizo, kampuni ya Yono, ilieleza kuwa itarudia mnada huo tarehe 24 katika maeneo ya nyumba hizo ambayo ni Mbweni JKT na Upanga. Za Mbweni ziko katika kitalu namba 47 huku ile ya Upanga ikiwa katika kitalu namba 701.
ANAVYOJIPANGA KIVINGINE
Licha ya kulazimika kuripoti Polisi kila uchao katika kipindi hiki anachochunguzwa na Polisi, Dk. Shika amekaririwa akisisitiza kuwa bado anazitaka nyumba hizo.
Akielezea juu ya kukamatwa kwake, alisema kilichomponza ni kutokuelewana tu na wauzaji kwa sababu yeye anategemea fedha zake zifike kutoka katika kampuni yake iitwayo Lancefort iliyoko Russia lakini wauzaji wa nyumba hizo walimtaka alipe asilimia 25 mara moja.
Aidha, Dk. Shika alisisitiza kuwa msimamo wake uko pale pale wa kwenda kulipia nyumba hizo na siku hiyo atawataka waendesha mnada huo (Yono), kuwaita waandishi wa habari na kushuhudia tukio hilo.
Hata hivyo, jana hakusema kama atahudhuria kwenye mnada mwingine wa nyumba hizo, bali akasisitiza namna alivyojipanga kivingine kwa kupokea fedha zake na kisha kwenda kulipa huku vyombo vya habari vikishuhudia.
Post A Comment: