Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki(CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.


Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi  amempongeza Nyalandu kwa kuwa ni alikuwa mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo.

Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia  uchaguzi wa madiwani katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.

β€œKuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka,”amesema Lissu leo Jumanne akiwa jijini Nairobi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: