
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Baada ya msemaji wa Simba Haji Manara jana kusema mwamuzi Elly Sassi aliwaonea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Novemba 28 mwamuzi huyo amejitokeza na kusema Haji Manara amekosa cha kuwaeleza Wanasimba.
Elly Sassi amesema Haji Manara anatakiwa kujua sheria za soka kwanza ndio aongee vinginevyo aende TFF akapate mafunzo ya kuwa mwamuzi sio kuangalia tukio moja kisha kulitafsiri kiushabiki.
“Nafikiri Haji Manara amekosa cha kuwaambia Wanasimba lakini matukio na maamuzi ya uwanjani siku ya mchezo hayana utata wowote kwa watu wanaojua sheria za soka ndio mana baada ya mchezo wakufunzi mbalimbali wa CAF walinipongeza”, amesema Elly Sassi.
Mwamuzi huyo ambaye amejizolea sifa miaka ya hivi karibuni kutokana na uchezeshaji wake ameenda mbali zaidi na kutafsiri kisheria matukio ambayo Manara anahisi yalipaswa kuwa penalti.
“Tukio la Yondani kisheria ni kweli alishika, lakini dhamira na namna ya tukio lilivyokuwa mkono haukuwa na mawasiliano na mpira na alikuwa ameruka juu katika harakati za kuokoa mpira ukafata mkono wala hakutumia mkono kuokoa mpira huo sawa na tukio la Tshishimbi”, amesema Saasi.
Post A Comment: