Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani mkoani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na siyo kumtishia mbunge huyo.


Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa mfululizo (series) wa matukio hayo yanayohusisha rushwa.

Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.

"TAKUKURU siyo mahakama na haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro

Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: