Winga wa Timu ya Taifa Stars, Simon Msuva amesema kwamba pamoja na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi katika mchezo wa kirafiki jana anaamini kwamba timu hiyo ilikuja kulipiza kisasi cha kipigo walichokipata katika michuanoCOSAFA iliyofanyika nchini Afrika ya Kusini lakini wameshindwa.


Akizungumza baada ya mchezo uliochezwa  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Msuva amesema kwamba wao walikuwa wamejiandaa kwa ushindi lakini haikuwa hivyo na hatimaye kuangukia kupata sare ya bao moja ambalo alilifunga yeye mwenyewe katika dakika 57 ya mchezo .

Katika mchezo huo ambao ulijaa purukushani za kutosha ulimpelekea Kocha wa timu ya Malawi kutolewa uwanjani kwa sababu ya kuvuka mipaka ya benchi la ufundi na kuingia uwanjani wakati mechi ikiendelea.

Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji wawili wa Taifa Stars, Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin  walitolewa kwa kadi nyekundu kutokana na makosa ya kimichezo yaliyoonekana na refa.

Kwa upande wa Malawi walitangulia kupata goli katika dakika ya 35' kupitia Nahodha wa kikosi chao Ng'ambi Robert ambapo alipofanyiwa mahojiano alisema "hajaridhishwa sana na goli alilopata kwani alitegemea kufunga magoli zaidi ya mawili"
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: