
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Katibu wa Bunge wa zamani, Dk Thomas Kashililah amesema, Rais John Magufuli hakufanya kosa katika uteuzi wa Katibu wa Bunge.
Rais Magufuli juzi Jumamosi alimteua Steven Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge, uteuzi ambao umeibua hoja kwamba sheria haikufuatwa.
Dk Kashililah akizungumza na mwananchi jana Jumapili, amesema kwa mujibu wa ibara ya 87(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mamlaka ya uteuzi haikufanya kosa licha ya sheria ya Bunge kuelekeza utaratibu.
Amesema, “Mamlaka ya uteuzi iko sahihi… unajua sheria haiko juu ya Katiba na Katiba iko juu ya sheria, hivyo Rais akiamua anaweza kufanya hilo, sheria haiwezi kumzuia,” amesema Dk Kashililah akisisitiza ibara ya 87 iko wazi.
Ibara hiyo inasomeka: “Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”
Dk Kashililah amesema: “Kama aliyeteuliwa angekuwa hayuko kwenye madaraka ya juu hapo sawa, lakini huyu aliyeteuliwa (Kagaigai) ni mtu senior kabisa serikalini na ana vigezo hivyo… kuna watu wanapotosha ukweli.”
Post A Comment: