Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani jana Septemba 12, wameendeleza mgomo kwa lengo la kupinga kuapishwa kwa Mbunge mteule wa Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa Nchini.
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Suzan Lyimo alisema wameamua kutoka nje baada ya kuona orodha ya matukio kuwa kuna Mbunge wa CUF anaapishwa.
Lyimo amesema kuwa wataendelea kususia tukio lolote linalohusisha wabunge hao wapya wa CUF.
Ndani ya CUF kumekuwepo na mgogoro kwa muda mrefu na kugawanyika kwa makundi mawili moja likiwa ni kundi linalilomuunga mkono Mwenyekiti huku kundi lingine likiwa ni upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.



Post A Comment: