ads

Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk amesema mgogoro wa madiwani wa CUF umemalizwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.


Mbarouk alisema Maalim Seif alikaa na madiwani hao jijini Dar es Salaam na kuwaamuru waingie kwenye vikao vya Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Mbunge huyo ambaye wiki iliyopita alituhumiwa na baadhi ya madiwani waliosimamishwa kuhusika kumchochea Meya wa Jiji la Tanga, Mhina Mustafa (Selebosi) kuwapa adhabu hiyo, alikanusha tuhuma hizo.

CUF ina madiwani 20 ambao kati yao, 12 waliamua kuingia kwenye vikao vya Baraza la madiwani mwaka jana na kutuhumiwa kukisaliti chama, lakini baadaye wenzao wanane nao waliingia huku wakilalamika kutengwa na kunyimwa stahiki zao.

Naye Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Mohamed Haniu (CUF) alisema kitendo cha madiwani 20 wa CUF kuingia kwenye vikao kimesababisha wenzao na wale CCM kuelekeza nguvu zaidi kwenye maendeleo
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: